Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

HISTORIA LYRICS - BY LADY JAYDEE

CHORUS:
Unakubalije uwe historia, 
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia, 
Kabla siku yako haijafika.

 VERSE 1:
Muda huo muda ulikuwepo
Muda huo uliopewa
Hela nazo zilikuwepo
Hela ulizo barikiwa
Maisha mazuri, nyumba nzuri
Gari zuri, na nini na nini
Muda huo uliuchezea
Pesa nazo ulizichezea
Kabla hata ya uzee haujaja
Wamesha sema aaah!! alikuwaga


CHORUS:
Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haija fika 

VERSE 2:
Tena hata, hata wenzio
Ulo kuwa nao jana
Hata nao wanakusema, mbali na kukucheka
Umegeuka story, umekuwa mfano
Umegeuka tukio, sio kivutio
Muda huo uliuchezea
Pesa hizo ulizichezea
Kabla hata ya kifo chako
Walisha sema aaah! alikuwaga


Rudia chorus:

BRIDGE:
Sitaki leo kuwa historia
Labda kesho iwe historia
Nataka niache historia
Itakapofika kuwa historia

Rudia chorus: 
 Wimbo Umeandikwa na : 
JUDITH WAMBURA (LADY JAY DEE)
Producer: MAN WATER
Studio: COMBINATION SOUND

HISTORIA VIDEO:
Tumemaliza utengenezwaji wa video ya Historia week end hii
Na iko kwenye hatua za editing.
Ni matumaini tutawapatia hii kama zawadi ya X-Mas na mwaka mpya na nyinyi mtaifurahia.
Ila kwa sasa chukueni hayo mashairi ili tukikutana kwenye showz msipate kazi kuimba pamoja na mimi