Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

SHUKRANI ZA DHATI KWA MAPENZI MLIOYAONYESHA TAR 14 JUNE 2013


Napenda kuchukua nafasi hii kutoa salaam zangu za shukrani kwa watanzania wote na wapenzi wa muziki kwa ujumla.
Kwa upendo na moyo mliouonyesha kuja ku support show yangu ya miaka 13 ya Lady JayDee pamoja na uzinduzi wa album ya Nothing but the truth.

Nilifarijika sana kuona umati mkubwa wa watu uliojitokeza bila kujali kuwa eneo lilikuwa limejaa
Nawaomba radhi pia kwa wale walioshindwa kuingia ndani.
Naamini yote hayo mliyafanya kutokana na mapenzi yenu ya dhati juu ya muziki huu.

Sina picha za ku post kwani picha zote zimesha postiwa kwenye blogs mbali mbali hapa nchini
Zaidi nitakuwa nafanya marudio tu ya ku copy paste, jambo ambalo si sawa kwa sasa.

Nawashukuru kwa kuzipokea nyimbo zangu zote mbili vizuri 1. JOTO HASIRA na 2. YAHAYA na kuziweka katika chart za juu kwenye radio stations zote ambazo hazina ubaguzi nchini Tanzania
Niwaahidi tu kuwa, nimerudi kazini rasmi na nitakuwa natoa kitu baada ya kitu.

Nitajitahidi pia kuendelea kuwa karibu nanyi, ili kupeana mawazo mbalimbali ya kujenga
Na pale kwenye mapungufu tushirikiane kurekebisha kwa pamoja.Kwa sasa nipo mjini NAIROBI - KENYA
kikazi kwa muda wa siku 5
Nitarejea Nyumbani Siku ya Ijumaa tuendelee na Sanya Sanya pale Nyumbani LoungeNikishamaliza kazi hii ilionileta, na nikiwa tayari nitawafahamisha ni kazi gani ila kwa sasa mta enjoy picha, Sina camera pia nimeisahau Dar.
Hivyo mvumilie kupata picha za simu yangu mbofu mbofu, ambazo hazina ubora wa hali ya juu

IJUMAA kuna Special appearance ya Patricia Hillary, muimbaji wa zamani ambae ndio alieimba original ya wimbo wa NJIWA peleka salamu.
Ni Nyumbani Lounge kuanzia saa 3:00 usiku
Lady JayDee na Machozi Band pia tutakuwa pamoja kuwapa burudani

Karibuni sana