Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

SEMINA YA KUWEZESHA WANAWAKE KUONDOKANA NA NJAA NA UMASIKINI, INAYOFANYIKA CHINI YA MFUKO WA FURSA SAWA KWA WOTE CHINI YA MAMA ANNA MKAPA

 
Semina hiyo inakayofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tar 25, 26 na 27 July 2013
Ni program inayowawezesha wanawake wajasiriamali kupata elimu katika kuondokana na umasikini na njaa.
Elimu kuhusu uzalishaji bora wa bidhaa, uundaji wa vikundi vya uzalishaji na kutafuta/ kuwapatia masoko kupitia mkakati kabambe wa maonyesho ya Sabasaba na mengineyo nsani na nje ya nchi.
 
Tangu kuasisiwa mwaka 1997 zaidi ya wanawake 3,650 wamehudhuria mafunzo na 2,500 kushiriki maonyesho.
Kuna wajasiriamali zaidi ya 630 wanaojitegemea katika biashara za ndani na nje ya nchi
 
 
Mwenyekiti wa mfuko wa fursa sawa kwa wote Mama Anna Mkapa akihutubia wanawake mbali mbali waliofika kuhudhuria semina hiyo.

 
Mheshimiwa mgeni rasmi akitoa nasaha zake, wakati wa semina hiyo
Iliofanyika katika ukumbi ulioko ndani ya eneo la JKT Mgulani, jijini Dar es salaama

 Picha ya Pamoja ya waliohudhuria hafla hiyo


Mwanamke mjasiriamali katika nyaja ya burudani na biashara Lady JayDee alikuwa ni mmoja wa wageni waalikwa katika kutoa hamasa kwa wanawake na burudani pia.

 Kuna program ya afya pia, ambayo imelenga kuboresha afya ya mama na motto kwa ujumla.
 
Kuna program ya elimu inayotoa changamoto za elimu kwa watoto na familia masikini
 
Kuna program ya ustawi wa jamii imelenga katika elimu ya haki za binadamu na watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu.
Na mafanikio ni kuanzishwa kwa kituo cha watoto yatima Kibaha Children's Village Center km 40 kutoka Dar es salaam mjini.
Kituo kimeanza kwa majaribio na kina watoto 9 na walezi 4.
Ujenzi unaendelea na usajili wa watoto unaendelea piaWanawake toka mikoa mingi ya Tanzania wamefika kujifunza na kuhamasika.
Wakiwemo wengine wengi waliofaidika na mfuko huo