Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

JINSI YA KUPIKA NYAMA YA NG'OMBE YA MCHUZI

Kabla ya nyama kuungwa na kuonekana kama inavyovutia hapo kwenye picha unatakiwa kupitia hatua zifuatazo

1. Unakata kata Nyama yako vizuri, unaiosha kisha unaipaka Limao kwa wastani halafu unaweka chumvi.

Weka jikoni ichemke kwanza bila kuongeza maji yoyote mpaka maji yake ya asili yakauke halafu ndio uongeze maji mengine ya kuilainisha.
Ongeza kiasi cha maji kwa kadri unavyoona ugumu wa nyama hadi ilainike

Kwa wastani haiwezi kuzidi dk. 20 - 30.

Ikiiva itoe jikoni na uiweke pembeni hakikisha haijakauka mchuzi wote, ibaki na mchuzi wake kiasi


2. Hatua inayofuata ni kuiunga nyama, hapa unaanza na mafuta kiasi unaweka kwenye chombo chako cha kupikia unaacha yachemke kidogo

3. Mafuta yakichemka unaweka vitunguu unaacha vikaribie kuwa brown ila usiunguze

4. Baada ya hapo unafuatiwa na Nyanya fresh zilizo katwa katwa vipande vidogo. Unafunika unaacha vichemke mpaka vipondeke kabisa kusibaki hata na mapande mapane.
Yaani liwe rojo zitoooooooo

5. Hatua ya mwisho ni kuweka nyama uliokuwa umeshaichemsha awali ndani ya mchanganyiko wa viungo hivyo unakoroga na ikiwa nzito sana unaweza kuongezea ile supu ya mchuzi uliobaki kwenye sufuria.

Ukipakua itaonekana kama ambavyo picha ya hapo juu inaonyesha.......
Unaweza kupika hivi kwa nyama ya Kuku na hata Mbuzi