Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

NYOTA NDOGO AKANUSHA MADAI YA GAZETI LA RISASI

Tofauti na habari ilioandikwa na gazeti hilo kuwa alijivinjari na mchumba wa mtu siku ya Valentine alipokuja kufanya show yake hapa jijini Dar es salaam.
Nyota amesema kuwa huyo ni bouncer aliekuwa amepewa kuwaangalia na kuwasaidia.
Na kuwa hata aletwe hapa leo hataweza kumkumbuka sura yake.
Hapo alikuwa anapewa msaada ili aweze kupanda jukwaani na si vinginevyo.
Nyota Ndogo anawaomba washabiki wa muziki wake hapa Tanzania na kwingine kote habari hiyo ilipoenea, kutoamini madai hayo yalio andikwa na gazeti kwa kuyakanusha vibaya sana.

Na anategemea kuondoka siku ya Alhamisi kurudi nyumbani kwao Mombasa, ila kwa sasa bado yupo Tanzania akimalizia kazi mbali mbali zilizomleta