Sikiliza nyimbo Zangu kwa Kudownload Mziiki App Bonyeza Link hii>> kwa kusikiliza na Kuenjoy!

MUNGU YU MWEMA
EID MUBARAK

Shukrani za dhati kwa Bi Zainab wa Said kwa chakula ki tamu.
GOD bless you

HORSE BACK RIDING -CHICAGO

Tukifika kwaajili ya kujaribu kitu kipya
Ambacho ni kuendesha Farasi.
Eneo ni kwa Sarah's Pony Rides mjini Chicago
Unatakiwa kujiandikisha na ku sign mkataba wa kuwa wakati unamuendesha farasi wako, ukipinduka ukaumia ni juu yako.
Bei ziko hapo kutokana na muda unaotaka kuendesha farasi,.
Kama ni mara ya kwanza au ya kumi lakini watu wote wanaofika kushiriki wanapewa maelekezo kabla ya safari kuanza.
Hapo ni pa kuanzia,  mnaelezewa weeeee kisha mnaanza kuondoka baada ya kuhakikisha kila mtu ameelewa jinsi ya ku ride

Tuli chagua safari ya mwendo wa saa nzima
Na tulihitimisha kwa kurudi pale pale tulipoondokea
My sister Janet ndio alinipeleka

 Mengine unaweza kuyaona kupitia Diary ya Lady JayDee #EATV #Sundays #9pm

JARIBU KULA HIVI KWA MIEZI ANGALAU 3 MFULULIZO TUONE KAMA HUTAPUNGUA


Mchana badala ya kujishindilia ugali au chips
Unaweza kusaga mchanganyiko wa matunda unayo ya pendant,  bila kuongeza maji
Yanatoka mazito kama mtoni,  ukinywa glass 2 tu hutasikia hamu ya kula chochote kile kwa jinsi tumbo litakavyokuwa limejaa
Add caption
 
Jioni badala ya kula wali na maharage,  unachukua mboga mboga unazi blend ukichanganya na tunda lolote tamu,  apple ama nanasi,
mboga unazoweza kutumia ni zozote zile za kijani.
Iwe,  mchicha,  spinach n.k


Unavisaga kwenye machine mpaka vinakuwa ujinga
Ili Kupata juice nzuri unaichuja Ili kuondoa makapi
baada ya hapo ni kunywa maji mengi tu, huna haja ya kula chakula kingine chochote kile
sababu hicho chenyewe ni chakula tosha

Ukishindwa kabisa kuzuia hamu ya kula
jisaidie kidogo kwa supu ya kuku au samaki
ambayo haijawekwa vitu vingi zaidi ya chumvi na limao au ndimu.
Fuatisha utaratibu huu kwa muda wa miezi 3
Uone matokeo yake

PIC OF THE DAY


DIARY YA LADY JAYDEE : SAN ANTONIO

Mambo ya kitalii,  mnazungushwa tu hapo kushangaa magorofa na hadithi za kufanya mliwe dola zenu
Hii sehemu inaitwa River Walk iko San Antonio Texas,  ni kwaajili ya watalii kama sisi
Paris kuna river km hii na idea ya kuzungushwa kwenye viboti na kuelezewa historia ya mji iko hivyo hivyo inafanana. 
Sijui nani kamuiga mwenzie? 
Basi bwana unalipa zako dola 9 unapanda kwenye hizo boti unapata ka tour ka takribani nusu saa hivi
Ukiamua una reserve boti mnaseviwa chakula humo humo ila hiyo gharama zake zinakuwa kubwa zaidi na inapendeza km mnakuwa zaidi ya watu 10-15 hivi as a family.  Ila kwa sisi watatu tulikaa tu na kupata dinner kwenye moja kati ya restaurants nyingi zilizopo eneo hilo
 Tulijichagulia chakula cha ki MexicanNa wakati mnakula mezani inapita band kutumbuiza, kama mkipenda lakini
kila wimbo mmoja dola kumi,  wanaijuaje hela sasa
baada ya hapo tulipata nao picha ya kumbukumbu
Na mengine utayaona kwenye Diary ya Lady JayDee
#EATV #Sundays #9pm

DIARY YA LADY JAYDEE : MUALIKO WA IFTAR NYUMBANI KWA BI ZAINAB KIBODYA

Kutoka kushoto ni Amina Lesso,  Jide na Magreth
Mgeni na mwenye nyumba Bi Zainab

Picha ya chini ni Mama Imelda Mutafungwa

Kwa maelezo zaidi ya picha kideo,  usikose kufuatilia kipindi kila jumapili saa 3usiku EATV
Marudio huwa jumatatu saa nane mchana

ALBUM YA PICHA ZA HARUSI YA FRANK NA ANITA MUTAFUNGWA -AMERICA

Maharusi wali badilisha nguo mara tatu

Miss Temeke , Miss Tanga na Amina Lesso .
Picha ya chini wa kati kati ni Zainab Kibodya

 
Luise nae alikuwa moja ya waalikwa 

With my Wifi Mage